Mnamo mwaka 1965
tulitoa kitabu chetu cha kwanza, “Muongozo wa Ibada za Kiroho”.
Wakati huo
kulikuwa kuna upungufu mkubwa katika soko la vitabu, katika
suala hili... Ilikuwa lazima kitabu hicho kitolewe katika wakati
ule ambapo vitabu vya dua visivyokidhi haja ndivyo vilikuwa
vimejazana.
Kwa kadiri ya
uwezo wetu tuliandaa kwa mtazamo uliozoeleka na kutoa kwa ajili
ya matumizi ya ndugu zetu wapenzi wa kiislam, kitabu cha dua
kidogo lakini chenye kujitosheleza
Sifahamu ni
kiasi gani kitabu hiki kilichochapishwa kwa wingi kimesambaa
Uturuki katika kipindi cha miaka mingi iliyopita katikati.
Lakini, sintoweza kushukuru vya kutosha kwa kiasi nilivyoona na
kusikia idadi ya watu na nyumba zenye kitabu hiki...
* * *
Katika utoto
wangu baba yangu alilete nyumbani kitabu cha dua kinachoitwa “REHBERİ
İBADÂTİL MANEVİYE” ... kama alivyokuwa mama yangu, kwa hamu
na shahuku nilikisoma na kujaribu kunufaika nacho katika
matatizo yangu mbalimbali. Mfano, nilikitumia kwa haja zangu na
kujiongezea imani. Na bila shaka faida zake nimeziona...
Nilipooa, baba yangu alininunulia kitabu kama hicho; na
ninaendelea kukisoma mpaka sasa...
Hiyo ni mistari
kutoka kwenye barua ya msomaji wetu ambaye ana watoto wakubwa tu
hivi sasa.
Naam,
Alhamdulillah, kitabu chetu kilipita kwa vizazi hadi vizazi;
kimepata daraja ya “Kitabu cha enzi”.
Hata hivyo,
katika kipindi cha katikati, kama matokeo ya utafiti wetu, na
kwa ufunuo wa muumba tumefahamu taratibu nyingi zaidi. Na
tumetaka kwa kadiri iwezekanavyo tugawane na idadi kubwa ya
waislamu ujuzi huu wenye faida...
Kwa upande
mwingine kinatakiwa kiwepo kitabu cha <<DUA na DHIKIRI>>
ambacho kitajibu maswali kuhusu mada hizi mbili kwa mujibu wa
elimu na ufahamu wa kizazi kinachokua.
Kitabu chetu cha
kwanza, kutokana na uzoefu mdogo ulioambatana na ujana,
tulikiacha chini ya udhibiti wa mchapishaji, kwa sababu ya kutoa
haki ya usambazaji... Hivyo basi safari hii, kwa uwezo wa Allah,
tunakitoa kama zawadi kwa ndugu zetu wote wa kiislamu. Kitabu
chetu hiki hakina haki ya usambazaji! Hakikuandikwa kwa ajili ya
pesa. Yeyote atakaye, kwa sharti la kuwiana na kitabu asili,
anaweza kunufaika na kitabu hiki na pia kuwanufaisha
wanaomzunguka... Anaweza kuwazawadia rafiki zake wa kiislamu.
Itakuwa vizuri sana kama akituombea radhi sisi kwa kusema
“Allah akuridhie” na kutusomea “Ihlas tatu na Fatiha
moja”...
Rasulu wetu
Muhammad Mustafa alayhi swalaatu wa sallaam, kiongozi wetu
kasema , “Atakayesaidia jema, anakuwa kama amelifanya jema
hilo”.
Naomba, Allah
atufanye tuwe wenye kusaidia mema katika uhai wetu wote; Atupe
hifadhi tusiwe vyombo vyenye kusababisha shari na kufanya
matendo yatakayotujutisha kesho...
Allah atujaalie
kunufaika na kitabu hiki, na atuwezeshe tuelewe thamani ya mali
iliyopo mikononi mwetu.
Asili:
Matamshi:
Laa ilaaha illallah
Maana:
Kiswahili:
Hukuna mungu,
Allah Pekee
Kiingereza:
There
is no GOD, only ALLAH
Kituruki:
Tanrı
yok, sadece ALLAH var