Rafiki yangu fahamu kwamba
kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vyenye thamani ulivyowahi
kupewa katika maisha yako.
Kitabu hiki ni wito kutoka
kwa RAB wako; ni ufunuo maalum! Bila kujali asili yako;kazi
yako ; shughuli zako; wala dini unayofuata, jua kwamba RAB
wako anakusubiri na mlango wake uko wazi kabisa kukupokea.
Usishangae ukauliza mlango
wa RAB wako uko wapi; mlongo “HUO” upo kwako; kwenye moyo
wako! Nyuma ya mlango unaofunguka kutoka kwako kuja kwako!...
Mlango huu ni mlango wa DUA
na DHIKIRI!... Ni mlango ufungukao kutoka moyoni mwako
kuelekea kwa RAB wako.
Ni mlango wa HAJA na
kumuelekea RAB wako!..
Achana na MUNGU unayemdhania kuwepo Mawinguni na kando
yako; Muelekee ALLAH asiye na mwisho wala mpaka;
Tambua kwamba YEYE yupo kila mahali katika kila chembe; na
jitahidi KUMTAFUTA ndani ya moyo wako!..
Kisha taka kutoka KWAKE
chochote utakacho!.. Mwenza, kazi, lishe;Ukipenda Mola,
ukipenda shifa!...
Fahamu kwamba kitu pekee
kitakachokufikisha kwenye haja yako ni DUA na DHIKIRI.
Rafiki yangu jua kwamba
ALLAH ambaye yupo katika kila chembe kwa sifa zake zote; na
ambaye hakuna kilichopo isipokuwa yeye, ATAKUJIBU KUTOKA
KWAKO KUJA KWAKO!
Ujue kwamba WEWE ni
“KHALIFA” katika ardhi!... Je unahabari kuhusu nguvu kubwa
zilizowekwa katika UBONGO WAKO kama KHALIFA? ...
Je unahabari kwamba unaweza
ukaufanyisha kazi mfumo ulio ndani yako kwa kutumia DUA na
DHIKIRI, na kwa kutumia UBONGO wako wenye sifa za ajabu?
Je unaujua mfumo wa dua
uliozawadiwa kwako kama “SILAHA YENYE NGUVU KABISA”?
Mafukara, wanyonge na watu
wengine wengi, kwa kutumia DUA na DHIKIRI, wamewaangamiza
WATAWALA wengi MADHALIMU!.
Kuna masikini wengi
wamepata utajiri mkubwa kwa kutumia DUA na DHIKIRI!...
Wapo wengi wenye matatizo,
dhiki, maradhi, mihangaiko na mateso wamepata uokovu na
afueni kwa kutumia DUA na DHIKIRI!...
Rafiki yangu fahamu
kwamba...
UNACHO kifaa ambacho ni
silaha yenye nguvu kuliko zote duniani.
Kwa kujifunza namna ya
kuitumia silaha hii yenye nguvu kabisa KATIKA UBONGO WAKO,
KATIKA MOYO WAKO unaweza ukafikia mazuri na mema yote ya,
hii dunia unayoishi na maisha ya baada ya kifo!..
Hali kadhalika unaweza ukaamua kutoutumia mfumo huu
wa DUA na DHIKIRI, ukauacha upate kutu na kuutelekeza, kwa
kufanya hivyo ni wewe pia ndiye utakayebeba adhabu yake
milele!...
Huu ni mfumo ambao wewe
umepewa bure!.. Ni zawadi!..
Humuhitaji mtu yeyote kwa
ajili ya DUA na DHIKIRI na wala huna ulazima kumtumia mtu
kama wakili!..
Ukitaka tumia kitabu hiki;
ukitaka elekea kwa namna unayoipenda mwenyewe!.. Lakini
hakikisha unajifunza namna ya kutumia kifaa hiki chenye
thamani kuliko vyote duniani cha DUA na DHIKIRI..
Utaona namna dunia yako
itakavyopendeza.
As Sayyid Ahmed HULÛSİ