Kuna baadhi ya
matendo yenye umuhimu mkubwa unapofanya DUA...
Unapofanya dua,
inabidi mikono uiweke mbele hali ya kuwa viganja vi sambamba na
uso na imeachaniswa kwa pembeni kuacha makwapa wazi. Inakuwa
yenye matokeo mazuri viganja vikiwa katika umbali wa kama
sentimeta 30 kutoka usoni hali ya kuwa kuna uwazi kati ya vidole
ili mionzi inayotoka katika kipaji cha uso iungane mbele na ile
itokayo katika vidole.
Tazama Rasulu
Alayhi swalaatu wasalaam anasema nini kuhusu hili:
“Mja yeyote akinyanyua mikono yake hali ya kuwa makwapa
yanaonekana na kuomba kwa ALLAH; dua yake itajibiwa kama
hatokuwa ni mwenye kuharakisha.
- Haraka
inakuwa aje ya Rasulallah?..
- Usema ,
nimefanya dua lakini haijakubaliwa”
(Anaachana nayo)... hili ni
kosa; Inabidi kuendelea mpaka dua itakapo fanikiwa.
Mionzi itokayo
kwenye ncha za vidole na mionzi yenye uelekeo maalumu itokayo
kwenye ubongo ni yenye umuhimu mkubwa katika kufanikisha jambo
pale inapoungana na kufanya athari za namna ya mionzi ya
LAZER.(Zaidi katika vitabu vyetu vya “Mtu na siri zake” na
”Utazamaji wa Mpweke”).
Kama
inavyobainika hapa, nguvu mama inayopelekea ufanikiwaji wa dua,
si yenye kuja kwa mtu kutoka nje; bali ni yenye kuzaliwa kutoka
kwenye nguvu ya kiroho ya majina ya Allah yaliyopo katika
uwepoji wa mtu.
Kwa kifupi DUA
ni zoezi lifanywalo na mtu la kufanikisha matakwa yake kwa
kutegemea nguvu za kiungu zilizo ndani yake.
Msingi wa DUA ni
“Mawimbi yenye uelekeo maalumu”...
Kama ambavyo
utokeaji wa awali wa ulimwengu ni udhihirikaji wa fikira ya
Allah kwa badiliko kutoka ukanda(dimension) wa elimu kuwa
nguvu(energy) na umbile la kikwanta, hata matakwa na matamanio
ya mtu yanatokea katika namna ya mkusanyiko, kwa msaada wa
mawimbi ya ubongo yenye uelekeo maalumu, wa matakwa na matamanio
ya ufahamu yatokayo katika ukanda(dimension) wa elimu.
Ni kwa sababu
hii basi jinsi daraja la kuyakusanya mawazo(concentration)
linavyoongezeka ndivyo hivyo hivyo majibu ya dua yanavyopata
kasi. Ndiyo maana imesemwa kwamba,
“Dua ya aliyedhulumiwa
haipotei; hapati faraja aliyepokea ah!
(aliyenung’unukiwa) !..”
Kwani, mtu
anayefanya “ah”, kwa machungu aifanyayo nayo; kwa
mkusanyiko wa mawazo aifanyayo nayo anaelekeza mawimbi negativu
ya ubongo kwa huyo mtu katika namna ya kwamba, inakuwa
haiwezekani hata kidogo mtu huyo kuukwepa mshale wa mawimbi
hayo...
Matokeo ya hiyo
“ah” kama hayakutokea kwa babu basi yatatokea kwa
mjukuu!.. Ki vipi? Rahisi tu!..
Mawimbi ya Ah
aliyoyapata babu, jinsi yanavyoathiri mfumo wake wa jenetikia,
hata kama matokeo yake hayatodhihirika kwake, yatadhihirika kwa
mtoto wake au mjukuu wake kutokana na mpokezano wa jeni; na
anakumbwa na adhabu ya babu yake. Ni kwa sababu hii ikasemwa,
“Babu kaiba tunda, meno ya mjukuu yemechomoka”.
Naam! Tumesema
viganja viwe mbele, mikono iwe imeachana katika dua... Kiongozi
wetu alifanya hivyo.
Hazrat
Rasulullah pamoja na
maswahaba walifanya dua hali ya kuwa wamesimama na viganja vyao
vimenyanyuliwa kama tulivyoeleza, dhidi ya wale waliotoweka
baada ya kuwauwa watu waliowakuta wenyewe jangwani wamejeruhiwa
na kuwasafisha majereha na kuwaponyesha; Watu hao walipatikana
baada ya muda mfupi sana na kupata malipo ya walilofanya.
Kama ilivyo kwa
dua ifanywayo kwa namna ya mawimbi “yenye uelekeo maalumu”
kwa msaada wa ncha za vidole hali ya kuwa umesimama na viganja
vipo kama tulivyoeleza vikitazama uso na mikono imelala kwa
mbele, dua inayofanywa katika hali ya kusujudu pia ina athari
kubwa sana.
Hasa dua
inayofanywa katika SIJIDA baada ya nusu ya usiku, yani muda
ambapo jua lipo nyuma ya mahali ulipo na mionzi ya jua iko
katika nguvu ya chini kabisa, ni yenye athari ya daraja la juu
sana. Kama dua hii itafanywa katika sijida ya mwisho ya swala ya
haja au swala nyingine yeyote nguvu ya athari inakuwa kubwa
zaidi...
Kama dua
itafanywa katika sijida ya mwisho ya swala, yani swala ya usiku,
baada ya kukiri mapungufu ya aina mbalimbali na kuomba
kusamehewa kutegemeana na kitu kinachohitajika, kama
utaendelezwa utaratibu huu kwa siku kadhaa bila kuacha au katika
namna ya kuendelezwa siku nzima; bila shaka kudura ya kiungu
itakubali kitu hicho kitokee.. Kwa sababu kuruhusiwa kwa dua
hiyo kufanyika kwa msisitizo namna hii ni ishara ya kujibiwa kwa
dua hiyo. Kwani, Allah huwa hatoi upenyo wa kufanyika kwa
msisitizo DUA ambayo hatoikubali.
Kama mtu si
mwenye kusisitiza katika jambo fulani, basi nafasi ya dua hiyo
kufanikiwa ni ndogo sana.
Temesema kwamba
dua ifanywayo katika hali ya SIJIDA, hasa ikiwa baada ya kukiri
makosa, huwa ni yenye nguvu ya hali ya juu sana... Kwa nini...?
Katika hali ya
SIJIDA, damu huenda kwa wingi kichwani na kwenye ubongo; ubongo
hulishwa vizuri sana na oksijeni na vyanzo vingine vya nguvu.
Kwa sababu hii basi unapata uwezo wa kurusha mawimbi yenye nguvu
sana.
Vile vile katika
hali hii ya SIJIDA huwa kunapatikana ukolevu wa mawazo na
uelekeo kwa kitendo cha kukiri makosa; hali hii inakuwa kama
chombo cha kufanikisha urushwaji wa mawimbi yenye nguvu katika
uelekeo wa kitu kinachohitajika.
Jambo muhimu
lenye kuipa nguvu na kuifanikisha dua ni kuwa mbali kwa ufahamu
wa mtu kutoka katika ukanda wa utawala wa nguvu ya WAHM
pindi dua inapofanyika... Na hali hii ni sijida yani
hali ambapo wazo la umimi linatoweka. Ndiyo maana Rasulullah
(A.S) akashauri DUA ifanyike “hali ya kuwa na uhakika
kwamba itakubalika bila shaka wala hofu”.
Nguvu kubwa
inayokata athari ya dua ni nguvu za WAHM wa WASIWASI
ambazo pia zipo kwa mtu mwenyewe...
Kiwango ambacho
WAHM na WASIWASI vimepungua kwa mtu, kinawiana na
ufasaha pamoja na uharaka wa kufanikiwa kwa dua ya mtu huyo.
Moja ya sababu
muhimu zilizolala katika kukubaliwa kwa dua za watu waliopata
yaqiin kwa ALLAH ni udogo wa WAHM na WASIWASI
walionao. Kwa upande mwingine hakuna shaka kwamba udhihirikaji
wa nguvu za kiungu katika maumbile yao, kama matokeo ya matendo
waliyofanya pamoja na upendeleo wa kiungu, pia ni jambo muhimu
lililopo katika kufanikiwa kwa dua zao kwa haraka.
Hali kadhalika
katika suala la DUA, MAJINI wanaojulikana kwa sifa ya
USHETANI wanakawaida ya kumpandikizia mtu fikira potofu sana
kiasi cha kumfanya asiitumie hii silaha yenye nguvu. Pindi
unapojisikia kufanya DUA, MAJINI wanaoitwa
SHETANI kutokana na sifa ya ushetani, bila kuchelewa
wanakupa wasiwasi...
“Kwa nini
nifanye dua, litatokea kama lipo kwenye kadari ...”
“Nifanye dua
au nisifanye dua lililopangwa ndilo litakuwa, kwa hiyo sina haja
ya kufanya DUA.”
Na hivyo basi
unaahirisha kufanya DUA, na kujinyima kutumia DUA ambayo ni
silaha yenye nguvu kabisa. Mambo unayokuwa umejikosesha
unapojinyima DUA kwa kutokufanya DUA, hayaelezeki wala
hayafikiriki. Ni kwa sababu hii basi, tazameni Rasulullah
(A.S) kashauri nini:
“Ombeni kila
kitu kuanzia viatu mpaka majani ya kondoo wenu kutoka kwa
Allah...”
“Ombeni
fadhila ya Allah, kwani anapenda kuombwa ”.
“Bila shaka
Allah anawapenda sana waja wake wanaofanya DUA kwa kusisitiza”.
“Jueni kwamba
kufanya DUA katika nyakati ambazo mnahisia ni bahati, kwa sababu
hali hiyo ni hali ya wakati wa rehema”
Maana
inayoashiriwa na hadithi ya mwisho ni hii ifuatayo:
Ikisemwa,
nyakati ambazo mnahisia, inamaanisha kuwa na unyenyekevu wa hali
ya juu kutokana na kukusanya mawazo kwa ukamilifu juu ya jambo
moja. Basi wakati huu unamaanisha uelekeo wa dhati wa mtu kwa
ALLAH. Uelekeo wa namna hii, kwa ubongo kujielekeza katika lengo
moja tu, unazaa ufungukaji wa nguvu za kiungu alizonazo mtu...
Jambo muhimu
kuliko yote katika kufanikiwa kwa DUA ni kubaki kwa HAQ kama
ndiye mwenye kusema hiyo DUA na mwenye kuleta hilo hitaji katika
ubongo wa mtu baada ya mtu kujitokomeza mwenyewe. Na hapa
inakuwa;
“Anapotaka
kItu kIWe, anasema kuwa nacho kInakuwa”
Moja kati ya
mambo muhimu saidizi katika DUA ni kuwa mng’ang’anizi juu ya
kitu kinachoombwa. Ni makosa makubwa sana kufanya dua juu ya
jambo fulani mara mbili-tatu halafu kuacha.
Inabidi uwepo
ung’ang’anizi katika jambo linalofanyiwa dua na inabidi kuwa
makini kwa kadiri inavyowezekana kwamba kitu kinachoombwa kiwe
chenye kulenga maisha yetu ya baada ya kifo na chenye faida.
Kwani, tunaweza kujiumiza vibaya kwa kukosea kuomba. Inafanana
na umeme, kama ambavyo tunaweza kuutumia kwa manufaa, hali
kadhalika tunaweza kuutumia kujiumiza au hata kujiua wenyewe.
Tumesema kwamba
Dua ni njia ya kujitambua kwa nguvu zinazomilikiwa na ALLAH
zilizopo katika uwepoji wako, uMIMI wako, NAFSI yako.
Hivyo basi kwa
kadiri tunavyoweza kuitumia kwa akili na ufasaha silaha hii,
ndivyo hivyo tutaweza kujilinda dhidi ya maadui zetu,
kufanikisha matakwa yetu, na zaidi ya hayo kupata yaqiin
kwa ALLAH...
Tumezungumzia
uzatitiwaji wa ubongo na nguvu za kiungu ndani ya kitabu chetu
cha “MTU na SIRI ZAKE”; Kwa kuelezea mfumo wake
tuliandika mwaka 1984 kwamba, hata ikibidi mawimbi ya ubongo wa
mtu yanaweza kusababisha silaha zisifanye kazi.
Tazameni namna
ambavyo hata Warusi, ambao si waumini, wanautumia ubongo hii
leo:
Tusome kwa
makini habari ifuatayo iliyoandikwa katika Gazeti la Sabah la
tarehe 11 Juni 1991 ukurasa wa 8.
“VITA VYA
BAADAE VITAKUWA VYA TELEPATHY
Mwanasayansi
maarufu wa umoja wa Sovieti Vlail Kaznatcheev, ameeleza kwamba
ubongo wa binadamu utakuwa unaweza kuathiri vita kwa njia ya
Telepathy. Prof. Kaznatcheev, anaendeleza utafiti ndani ya
maabara maalumu iliyoundwa ndani ya Novossibirsk Akademy ambayo
ni taasisi iliyokusanya watu wenye vipaji vya hali ya juu.
Profesa
Vlail Kaznatcheev ambaye pia ni mmoja wa wanachama wa Taasisi
ya sayansi ya Sovieti mjini Mosko, ameeleza kwamba ubongo wa mtu
unaweza kuathiri watu, mawazo na vifaa vya elektronik vilivyopo
hata mahali ambapo ni mbali sana kutoka mahali ulipo mwili.
Kaznatcheev
ambaye ameingia kwenye utafiti wa hali ya juu ili kuthibitisha
maoni yake haya ambayo yanachukuliwa kama maneno ya mwendawazimu
na watu wengi, amevutia wengi nchini kwake huko umoja wa
Sovieti. Serekali ambayo imempa wasaidizi pamoja na maabara
yenye vifaa maalumu ndani ya taasisi iliyolea watu wenye vipaji
vya hali ya juu, inamatarajio makubwa kutoka katika utafiti wa
Kaznatcheev.
Ulinzi wa KGB
Sifa kubwa ya
utafiti wa Kaznatcheev ni kujaribu kutumia nguvu ya ubongo wa
mtu kwa njia ya Telepathy kama silaha. Kwa mtazamo wake,
kwa kutumia nguvu ya kufikiria peke yake inawezekana kuharibu
mitambo ya kompyuta , rada za viwanja vya ndege, hata silaha
zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Serekali
ambayo inafuatilia kwa karibu utafiti huu imeunda kikosi cha
mashushushu kabambe wa KGB kumlinda Kaznatcheev asitekwe na CIA.
Mwanasayansi huyu mashuhuri anafafanua maoni yake kwa mifano
rahisi kabisa:
“Kama
kompyuta unayotumia imeharibika ghafla, usikimbilie kuwalaumu
watengenezaji . Stress uliyonayo au hasira zako, hata
kidogo wakati unaitumia, inaweza kuathiri mitambo. Kwa sababu
Ubongo wa mtu wa kawaida tu, unanguvu ya juu zaidi ya kompyuta
na mara nyingine mtu anaweza kuzitumia nguvu za asili alizo nazo
bila kujijua”
Kwa mujibu wa
Kaznatcheev, iwapo mtu amemuwaza sana mtu mwingine ambaye
hajaonana nae muda mrefu, na mara akapata simu au barua kutoka
kwake, asidhani kwamba hiyo ni bahati. Hii imesababishwa na
kumuathiri mtu anayemfikiria kwa mawazo aliyonayo.
Kaznatcheev,
kwa mara ya mwisho katika kipindi cha TV alichoshiriki
aliuonyesha mmea mmoja uliopo katika maabara yake na kuuonyesha
kwa muda mrefu na kuwapa watazamaji muda wa saa moja wafikirie
ukuwaji wa mmea huu. Matokeo yake kweli yalikuwa ya
kustaajabisha, ndani ya muda mfupi, mmea ulionyesha ukuwaji ya
hali ya juu.
Kwa upande mwingine
utafiti wa Kaznatcheev unalenga katika kuivumbua hali isiyo na
mpaka ya nguvu ya mawazo. Kaznatcheev ambaye anaendelea na
utafiti wake wenye lengo la kufika kwenye ufahamu wa ndani
(subconscious) wa mtu kwa kuunganisha sayansi na parasaikolojia,
amesema kwamba uvumbuzi wake utazaa matokeo muhimu sana kwa
ajili ya kufadhaisha mitambo ya maadui; na kwamba pamoja na hilo
yeye sio mwenye kuchochea jambo hili litumike kama silaha, bali
kama kitu cha kupoza na kuzuia vita.”
Ni kwa sababu hii
basi, DUA inaweza kuelezwa kuwa ndiyo nguvu ya hali ya juu
kabisa aliyotunukiwa mtu.