Rasulullah
Muhammad Mustafa alayhissalaam anasema “DUA NI SILAHA YA
MUUMINI”. Halafu anafanya ufafanuzi mwingine kuhusu “DUA”
kama ifuatavyo:
“DUA NI KIINI
CHA IBADA”
Tujikumbushe aya
ifuatayo baada ya hadithi hii:
“NIMEWAUMBA MAJINI NA WATU ILI WANITUMIKIE”
Kwa maana rahisi kabisa utumwa ni dua na dhikiri!.
Kwa maana pana utumwa ni ufanikishaji wa kiumbe wa lengo la
uwepoji wake...
Hivi tukifanya
dua itakubalika?..
“Kama mtumwa wangu atanyanyua mikono na kufanya dua, naona
haya kuirudisha mikono yake ikiwa mitupu.”
Naam, hii ni Hadithi Qudsi... Hadith Qudsi nyingine juu
ya jambo hili inasema:
“Ewe
mwanadamu, dua hutoka kwako jibu hutoka kwangu; istighfar hutoka
kwako na kusamehe hutoka kwangu; toba hutoka kwako kukubali
hutoka kwangu; shukurani hutoka kwako, kutoa kwa wingi hutoka
kwangu; subira hutoka kwako, msaada hutoka kwangu... Kipi
umetaka sikukupa...”
Ifuatayo ni aya inayosherehesha hadithi Qudsi hiyo:
“FANYENI DUA KWANGU, NIJIBU”
Kuna hadithi Qudsi nyingine yenye kufafanua suala hili:
“Mimi nipo
kwa mujibu wa dhana ya mja wangu. Basi afikirie atakavyo!..”
Yani, mnapofanya
dua, kama mkifikiria kwamba dua hiyo itakubalika basi mfahamu
kwamba mnachotaka kitatokea!..
Kwa mlengo huu,
mmoja wa mawalii wa ALLAH wa daraja la juu Imam Rabbani Ahmed
Faruk Serhendi amesema hivi:
“Kutaka kitu
inamaanisha kukipata kitu hicho; Kwani Allah taala hamuachi mja
afanye dua ambayo hatoikubali.”
Kimsingi,
tutakapotaka kitu kwa namna ya kufanya dua, inatakiwa tukumbuke
aya ifuatayo:
“ALLAH ASIPOTAKA NINYI HAMUWEZI KUTAKA”
Suala ni kwamba,
ombi litokalo kwako limetoka kwa sababu Allah kataka!.. Kama
Allah angekuwa hakutaka hata ninyi msingeweza kutaka.
Kitu kilicho
rahisi, cha bure na chenye athari kabisa ni DUA. Ni kwa sababu
hii basi DUA imeitwa “silaha ya muumini”
Ni namna gani
DUA inakuwa silaha ...
Ili kuweza
kuelewa hili inabidi kubobea katika tasawwuf...
Mtu kwa uhakika
wake ameumbwa kwa sifa za kusudio la jina ALLAH, yupo thabiti na
katika hali ya kudumu kwa kutegemea uwepoji WAKE...
Yu hai, anaishi
kwa sifa ya UHAI inayokusudiwa na jina la ALLAH la “HAYY”...
Ni mwenye elimu
na ujuzi akipanga maisha yake kwa sifa ya ELIMU kama
inavyokusudiwa na jina la ALLAH la “ALIM”...
Na ni mwenye
kufanya matakwa yake yafanikiwe kwa jina la ALLAH la “MURID”...
Hivyo basi mtu
anapata atakayo na kuondokewa na hofu ya anavyoviogopa kwa
kiwango kinachowiana na alivyo kadiriwa kudhihirisha maana za
majina haya ambayo yapo katika uwepoji wake...
* * *
Dua
ni nini?
Je niombi kwa Mungu aliye kando/mbele yako?..
Ama ni ombi la
kubainisha nguvu ya ALLAH aliye katika kiini cha uwepoji wako,
katika namna zote za uwepo wako, ambaye uwepoji wako unamtegemea?..
DUA, si kingine zaidi ya mbinu ya kudhihirisha nguvu za kiungu zilizopo
katika uwepoji wa mtu!..
Ni kwa sababu
hii, mtu akifanya DUA kwa dhati, ataona yanafanikiwa yale
yaliyokuwa yakionekana hayawi.
Ndiyo maana
basi, silaha ya mtu yenye nguvu kabisa ni DUA ...
Kama tunataka
kupata matokeo mazuri ya DUA, kwanza inabidi tuyape umuhimu
mambo kadhaa kuhusu namna ya kufanya dua, mahali pa kufanyia
dua, na wakati wa kufanya dua.