|
Je
sunna ni ndevu, masharubu, nguo, kilemba, au muonekano wa mavazi?
Hivi
nini yawezekana kuwa ndiyo Sunna ya Rasulullah?
Sunna
ya Allah yani SUNNATILLAH ni nini?
Wenye
ufahamu mdogo wanajua sunna kuwa ni operesheni wanayofanyiwa watoto wa kiume.
Ufahamu wa sunna wa wenye ufahamu wa wastani ni mpana kidogo... Kwao, sunna ni
Ndevu, masharubu na mavazi!... Kwao, kumfuata Rasulu wa Allah ni kujitumbukiza
katika mavazi ya miaka 1400 iliyopita; kufuata mila na desturi za kipindi
hicho!..
Hawa
ni waislam wenye kusema kwamba wao ndiyo waislamu na wale wenye kuvaa mashati ya
mikono mifupi si waislamu!
Hawa
ni kama waislamu waliomuua Kiongozi wa Uwalii, Mlango wa elimu Hazrat Ali!...
Ufahamu wao, ni ufahamu uliomuona huyu swahaba mkubwa ametoka nje ya dini!.
Tafitini yaliyosemwa na Hazrat Muhammad alayhissalaam kuhusu Hazrat Ali...
Muelewe hali na kiwango cha ufahamu wa waislamu ambao walimuona yu nje ya njia
ya Rasulullah!
Watofautisheni ambao, kwa madai ya kuhudumia dini na sunna wamefanya dini ufalme
na wamekuwa wakiitumia DINI kutawala watu.
Nimeamua nilifafanue jambo hili wazi wazi baada ya kuona habari kwenye ukurasa
wa internet ulionukuu ufafanuzi nilioufanya!
Nawaomba mfikirie vizuri nitakayoyaeleza...
Nilipokuwa na miaka 20 yani miaka 40 iliyopita, nilimuota Rasulullah
akaniambia niende kwa Hazrat Abubakar... Kilichofuata si muhimu hapa...
Na mimi baadae mwaka huo nikaandika maisha ya Hazrat Abubakar... Baadae
nikaandika kidogo maisha ya Hazrat Rasulallah ya kipindi cha Makka kwa
kuambatanisha na hadithi katika kitabu nilichokiita “Muhammed Mustafa”
alayhissalam.
Nimeandika haya kwa sababu ifuatayo. Nilitafiti kwa undani sana maisha ya wakati
huo... Nilisoma karibu Hadithi 60 sahihi.
Kama
inavyojulikana Rasul wa Allah Muhammed Mustafa alayhissalaam alizaliwa ndani ya
kabila la Kureishi lililokuwa na upapatikiaji wa Masanamu... Babu, na ndugu zake
wengine walikuwa wenye kufuata taratibu za kabila...
Rasulullah akakulia humo... ALIVAA kama wao, ALIACHA NDEVU kama wao, ALIFUNGA
KILEMBA kama wao!. Alikaa, kusimama, kula na kunywa kama wao...
Aliendelea hivyo mpaka alipofikisha miaka 39 akawa Rasulu wa Allah!... Kama
Rasulu wa Allah alibaini ukweli katika umri huu; Ulipokamilika UNABII miaka
mitatu baadae, akaanza kuwafahamisha watu yakufanya kwa mujibu wa Wahyi
aliopata, ili wajichumie kwa ajili ya maisha yao ya milele.
HAKUBADILI NDEVU WALA MAVAZI YAKE katika kipindi hiki wala baada yake!
Aliendelea kufunga kilemba kama wao, alivaa kama wao, na kuzunguuka na ndevu
kama wao!. Hata ile nguo yake yenye rangi nyingi na bakora yake aliendelea
nayo!..
Sunna
ya Rasulu wa ALLAH ni sunna ya makusudio ya jina “ALLAH” ambaye ndiye Rasulu
wake; “SUNNATILLAH”!.
Hata
sisi tukiielewa “SUNNATILLAH” na kuifuata tutakuwa tumeifuata sunna ya
Rasulullah na tutakuwa kwenye “SUNNATILLAH”! Lakini si kwa ndevu, masharubu,
nguo na vilemba!
VILEVILE JAMBO MUHIMU LINALOBIDI LIBAINIKE NI:
Rasulullah hakuingilia wala kuwashauri kuhusu mavazi na desturi wapapatikia
masanamu wakina Abu Jahil, Abu Lahab na mfuwasi wao ambaye alimuua mjukuu wa
Rasulullah, Yazid; Aliendelea kuwa ni mwenye kuvaa kama wao. Kwa sababu
hili halikuwa na umuhimu katika kufanikisha yanayotakikana na DINI; na wala
halina uhusiano na ukweli wa maisha ya milele au kujulikana kwa makusudio
ya jina “ALLAH”
Na hii
inamaanisha kwamba...
ALLAH akimuongoza mtu, mtu huyu anaweza akaendelee kuvaa kwa mujibu wa mila na
desturi za jamii yake, lakini hatofuata jamii yake katika mambo yanayohusika na
“SUNNATILLAH”; Na ataendelea kuufahamisha ukweli aliojifunza unaohusika na
uongofu alioupata!.
Hii
inamaanisha, si kupinga mila na desturi katika mambo
kama mavazi, bali kuendelea nayo ndiyo SUNNATIRASUL!.
Kwa
sababu DINI haikuja kwa ajili ya mapinduzi ya muonekano wa mavazi ya watu! Si
kazi ya Dini kushughulika na muonekano wa mavazi. Kwa mujibu wa suna, watu wana
haki ya kuvaa, kusoma, kuishi, na kufanya kazi kufuatano na imani zao bila
kuharibu amani ya jamii! Hata kama hili litakuwa liko kinyume kwa wale ambayo
mbongo zao hazijaelewa!
Kutoa
hukumu juu ya dini ya mtu kwa kuangalia mavazi yake ni ishara tosha ya mtu
asiyeendelea mwenye ubongo wenye kufuata mkumbo.
Rasulu wa
kusidio la jina “ALLAH”, kwa kuwafahamisha watu ukweli wa
utaratibu na mfumo wanaoishi ndani yake, alijitahidi kuwafanya waishi kwa mujibu
wa mfumo na utaratibu wa ALLAH ambao ulipewa jina la “DINI”, na hivyo
basi kuwa wenye kujiandaa na maisha ya milele!
“MTU WA DINI” ni
yule aliyetafiti, kuuliza na kuuelewa utaratibu na mfumo wa ALLAH na
kukubali kuishi kwa mujibu wake!. MTU WA DINI kutokana na mfumo huu aliouSOMA
anakuwa “MUTTAQI” yani mwenye kuchukua tahadhari dhidi ya hatari
zinazokuja alizozibaini!.
Kufuata sunna ya Rasulu wa Allah maana yake ni kuuthamini ufahamu wake, kudumu
katika njia aliyoionyesha na kwa kufanya aliyosema kufikia mambo mazuri
yanayokuja. Maana yake ni kuuvumbua uhakika wa kiini chake; na kufanikisha
matokea yake ya kusisimua!. Sio kufuja maisha kwa kufuata mkumbo.
Kufuata sunna ya Rasulu wa Allah maana yake ni
kuchanga na watu bila malipo elimu aliyozawadiwa. Siyo kuwaliwaza
watu na riwaya za muonekano wa mavazi!.
Mtu
aliyeuelewa mfumo na utaratibu wa Allah yani “SUNNATILLAH” na kisha akafanywa
yanayopaswa anakuwa ndiyo mtu aliyefuata “SUNNATIRASULULLAH”!.
Onyo
la kwamba “Atakayejifananisha na kundi lolote basi atakuwa miongoni mwao”
linamaanisha kwamba mtu yupo katika jumuia ambayo anachangia nayo Fikira na
Imani... na si ufanano wa mavazi au ndevu!.
Kama
tulivyo eleza katika makala yetu yenye kichwa “Kutawala watu kwa kutumia dini”,
kuna baadhi ya watu wamepiga marufuku udadisi na utafiti wa DINI; na hivyo basi
wamepelekea ukuaji wa watu wenye mbongo kama kaseti, wenye kuiga na wasio na
uwezo wa kufikiri.
Dunia
ni pahala pa hekima na kila ufafanuzi wa Rasulullah umelala kwenye hekima
fulani!. Mtu mwenye akili ni yule mwenye kuuliza na kutafiti kila jambo ili
kumuelewa vizuri Rasulullah na kujaribu kuifikia hekima ya
lililofundishwa.
Hili
limeashiriwa na onyo la kwamba “hekima ni kitu kilichopotezwa na mumin”
Yeyote aliye na mgongano wa mawazo au mapengo katika mfumo wake wa kufikiria, ni
mfuata mkumbo ambaye hajailewa dini na hajaweza kuuSOMA ufanyajikazi wa
utaratibu na mfumo aishio ndani yake.!.
Ukweli ni kwamba DINI haikubali ufuataji mkumbo!.
Kuiga matendo kunazaa matokeo yanayofanana; lakini hili
haliwezekani kwa kuiga mawazo
!.
Kuwa “Faqih” yani mwenye ueleo, ni Lutufu(upendeleo) ya Allah. Hivyo mtu anaacha
kuwa mwenye kufuata mkumbo.
Hata
siku moja kukumbuka kanuni za FIQIH hakumaanishi kuwa “FAQIH”.
Uwezo wa kuhifadhi vitu kichwani umepoteza thamani baada ya uvumbuzi wa kaseti!.
Dini imefahamishwa kwetu kuwa ni yenye kustahili kusomwa ili ubaini utaratibu na
mfumo unaoishi ndani yake; la muhimu zaidi “UJIFAHAMU
MWENYEWE”
! Uivumbue hazina iliyo katika uhakika wako; Na mwisho
ufahamu kusudio la jina ALLAH kwa mujibu wa elimu ya holografia na kuijua nafasi
yako katika ulimwengu..
Wale ambao hawajalielewa hili katika maisha yao hawajaisoma
“IHLAS”
Hata kama wameirudia mara laki!...
Tulifikirie vizuri onyo la Rasulullah kwamba, “Kuna
mwenye kuswali sana lakini hajaambulia lolote isipokuwa uchovu; kuna mwenye
kufunga sana lakini zaidi ya njaa hajapata faida yoyote”
Rasulu wa Allah ametufahamisha Quran ili tuielewe na kutafakari. Tufanye hivyo
hadi ufike wakati ambao hatua zote tunazochukua maishani ziwe zenye kuwiana na
SUNNATILLAH! Tusizungumze kipuuzi juu ya nywele, ndevu, mavazi, Rasulu hakuja
ili tupoteze umri kwa hukumu zinazohusu watu.
Je ni upi ufahamu wa dini unaoingilika kwa kusema kwamba
hakuna mungu wala wazo la
uungu
pamoja na Kusudio la jina ALLAH. (La ILAHA ILLA ALLAH)?
Wanaofuja umri wao kwa kuiga bila kudadisi wala kujaribu kuelewa hili; watapigwa
na bumbuwazi na kupata majuto makubwa kama matokeo ya kushindwa kuisoma hazina.
Inasikitisha kwamba ndani ya huu mfumo hakuna wazo la kufidia!.
Tahadhari:
Huu ni mtazamo wangu binafsi; Haumlazimishi yeyote yule kuufuata; Apendae
atachangia, asiyependa hatochangia. Kuna baadhi ya watu, kutokana na kuwa
tofauti na matarajio yao wanadai kwamba tunachanganya vichwa na wanapiga
marufuku tusisomwe kwa kusema kwamba
“tunawafanya watu
wafikirie na hivyo tupigwe marufuku”.
AHMED HULUSI
19 May 2005
NC, USA
|