|
Ndani ya
ufahamu wa dini unaoegemea kwenye wazo la Mungu, unadhaniwa kuwepo usiku
ufuatao ambao wanauita “Usiku wa Qadir”...
Mungu aliye mkubwa,
ameandaa neema kwa watumwa wake aliowachagua katika ardhi!.. kwa ajili ya
kuwalipa wale wanaompapatikia sana. Neema hiyo kubwa ameiita “QADIR”...
Malaika wanaoileta
(!) hiyo neema, wanashuka kwenye kitongoji wanachoishi waislamu ndani ya usiku
mtakatifu wa maadhimisho, - Kwani, huangamia wakiona mwanga; Kwa mfano wa
vitamini C iliyopata mwanga!..
Ndiyo hiyo “Qadir
isiyouona mchana”(!) ambayo ni kitu (!) kilicho bora kuliko upapatikiaji wa
miezi 1000, yani miaka 83.
Kila mwaka tarehe
27 mwezi wa Ramadhani, Malaika wakiwa na amri ya Mungu Mkubwa, hushuka
umbali wa miaka mingi kuelekea Duniani kwa kasi, huku wakichapa mabawa yao, na
kuanza kuwatafuta nyumba baada ya nyumba watumwa wanaofanya upapatikiaji katika
eneo ambalo ni usiku wakati huo.
Wakati huo basi
wale wote wanaoishi mahali ambapo ni mchana hawaambulii chochote!
Kwa mujibu wa
vigezo walivyonavyo mkononi, kama watampata mpapatikiaji muadilifu, bila
kuchelewa humuuliza mola wao, “Je huyu tumpe QADIR?” ... Kama
Mungu ataidhinisha, bila kuchelewa mtumwa huyo hupewa “Qadir”. Shughuli
hii ya utafutaji nyumba baada ya nyumba au, ya kugawa hii “Qadir”
inaendelea hivyo mpaka jua linapochomoza.
Haijulikani idadi
ya watu watakaopewa “Qadir” usiku huo!. Haijulikani vile vile kinachobadilika
kwa watu wanaopewa “Qadir” !... Mionzi ya mchana inapooneka malaika
pamoja na roho, bila kuchelewa, hurudi kwenye viota vyao vilivyopo kando ya
Mungu mkubwa!.
Katika kipindi
hicho, watumwa walioamini wanazunguka msikiti baada ya msikiti, wakitarajia
kubahatisha zawadi hii katika msikiti mmoja wapo!.
...
Kwa mujibu wa
ufahamu wa “DINI” unaoegemea kwa Rasulu wa Allah Muhammad Mustafa
aleyhissalaam, kwa mujibu wa watu tunaowaita Ahlullah ufafanuzi au uchanganuzi
wa kinachoelezwa kama usiku wa “Qadr” ni huu ufuatao:
Tumeubainisha
katika ufahamu wa mtu “Mjumuiko wa siri” unaokusudiwa na jina Qur’an
pamoja na “Asili yake iliyopo katika kiini chake” (Anzalna HU),
ndani ya kipindi ambacho mtu huyo anaushuhudia u”potea”ji (Layl)
wa uwepoji wake. Yakumbukwe maelezo ya kwamba “Qur’an na Mtu ni mapacha”.
Je unajua ni nini
hii asili au siri (Qadr)?
Giza la u”potea”ji (Usiku) ambalo ndani yake inafanikiwa hali ya Qadr,
ni lenye heri kuliko yanayoweza kufanikishwa katika kipindi cha miezi 1000 (Muda
wa uhai wa mtu wa karibu miaka 80).
Malaika(nguvu
za kimalaika – mabawa yanakusudia idadi 2-3-4 ya uelekeo wa ufanyaji kazi wa
nguvu hizi) na roho(maana ya asili, u’yeye’ “HU” wa uwepoji wao) ,
hubainika katika ufahamu wa mtu kulingana na idhini (uwanja wa
kufanikisha mambo - uwezo) ya Rabb wa mtu (muunganiko
wa majina (Asma) – muunganiko wa majina ya Allah yanayofanya uwepoji wake)
huyo; na hivyo basi katika muda huo, kwa kujumuisha na hisia ya u”potea”ji
wake, atamuhisi na kumbaini “ALLAH” ambaye yupo kwa ukamilifu! Mtu huyu
atakuwa ndani ya u“Salaama” kutokana na
kila aina ya hukumu!.
Hali hii huendelea
mpaka hisia na fikira za uwepoji, utu zitakapozidi uzito (anaporudi ALFAJRI).
Uwezo huu utafuteni
usiku wowote katika mwaka, yani, katika kila hali ambapo mnaweza kuuhisi u”potea”ji
wenu ndani ya enzi ya kusudio la jina ALLAH!... imedokezwa, “Utafuteni usiku
wa Qadr ndani ya kila usiku katika mwaka.”...
Imedokezwa, “Utafuteni ndani ya Ramadhani”
...jaribuni kuipata hali hii katika kipindi ambacho mnafanya jitihada za
kujikwamua kutoka kwenye utu na kuihisi asili yenu kwa
funga inayofanikishwa kwa maana ya kweli!
Imedokezwa, “Utafuteni
siku za mwisho za mwezi wa Ramadhani”... Utafuteni katika hatua za mwisho za
utakaso wa kiroho unaopatikana kama matokeo ya ufanikishaji wa funga ambayo
si ya kuiga bali iliyo ya uhakika!.
Sasa ngoja nijaribu
kuelezea kwa ujumla yale tuliyoyaelewa kutoka katika maelezo ya ufananishaji kwa
kutumia ishara ndani ya “Suratul Qadr”:
Kuna
muda (Muda wa Qadr) ambao ni wenye heri zaidi kuliko anayoyafanikisha mtu katika
kipindi cha uhai wake; Ndani ya huu ufunuo au mlipuko wa muda mchache katika
ufahamu, taharifa kuhusu asili yake zinashuka (Tanazzul), yani zinafunguka
“kutoka katika kiini chake kuelekea kwenye ufahamu wake” !.
Hii ni asili ya (uhakika wa) u’yeye’ wa “HU”.
Uhakika huu, kwa
mujibu wa kanuni inayosema, “Mtu ni siri ya Qur’an; Qur’an ni siri ya Mtu” ,
unafunguka kutoka ndani ya mtu!.
Wakati gani?
Mtu, baada ya
kuanza kwa kujiuliza mimi ni nani, kumuamini Rasulu wa Allah Muhammad
alayhissalaam, kuelewa aliyoyaleta na kwa kujikwamua(kujitakasa) kutokana na
wazo la Mungu, kuelewa kusudio la jina “ALLAH”, kimsingi kwa kiwango
kilichoelezwa ndani ya Sura ya “Ihlas”
... anapotumbukia katika kiza la kuuhisi u’potea’ji wake,
katika enzi ya aitwaye kwa jina pekee la ALLAH, kutoka katika uwepoji wa utu
wake, yani mwangaza wa mchana; na vyote vilivyopo, kupoteza uwepoji wake katika
uonaji wa mtu huyo...
Ndani ya muda
anapohisi na kubaini kwamba sifa za majina ya Allah ambazo ni kiini chake
(uhakika wake) ndizo zinazofanya uwepoji wake, atapata udhahiri na atafahamu
kwamba ROHO, yani maana ya majina haya pamoja na Malaika, yani nguvu za majina
haya ni zenye kudhihirika katika maumbile yake kila wakati!..Kulihisi na
kulibaini hili ndiyo hali ya “QADR”.
Ndani ya muda huo
hatobaki mwenyewe, wala kachembe kutoka katika vionekanavyo vipo...
Atashuhudia ukweli
unaoelezwa kwamba, “Je umiliki ni wa nani ndani ya muda huu (Yawm)?” “Lillahil
wahidil Qahhar (Ni wa Allah ambaye ni Vahid na Qahhar)”!. Atai”SOMA”
“Ash’hadu...”!.. Mwenye kutazama anakuwa yeye mwenyewe!
Hali hii,
inaendelea kwa huyo mtu hadi atakapojifahamu tena katika ukanda wa
kiutu(Alfajri). Hivyo basi anakuwa miongoni mwa wale waliofanikiwa kuubaini
uhakika wa uwepoji wao na baada ya hapo anaanza kuzi”SOMA” siri za Qur’an na
anakuwa ni mwenye kusubiri mauti ( badilisho lake la ukanda – dimension) na
wakati huo huo anakuwa ni mwenye kuendelea na “UTUMWA – UJA ” wake katika
namna inayowiana na lengo la kuumbwa kwake.
Kwa nini
tumeliandika hili?...
Nimeandikia ili
nichange nanyi ukweli wa kwamba,“Kitabu” kinachoelezwa kama “Kitabu
cha Amri za Mungu”, kwa mtazamo wetu sisi kinabeba maana ya “KITABU
CHA SIRI” ambacho ni tofauti kabisa; na kwamba bila kujifunza u”SOMA”ji
wake, kuna mambo mengi yatakosekana...
Huu ni mfano mmoja
... Ukianza na “MI’RAJ” kuna mifano kama hiyo mingi tuu ambayo inabidi
ifafanuliwe, ndani ya HICHO Kitabu ambacho ni Usemaji (Qalam) wa Allah!...
Inasikitisha kwamba
hata roho za wengi wetu hazina taharifa yoyote kuhusu haya!!! Bado tunadhani
kwamba Qur’an Karim ni kitabu cha historia na amri za mungu!...
Katika uchanganuzi
huu naweza kuwa niko sahihi, au nimepotoka!. Lakini hivi ndivyo tulivyosoma
kutoka katika vitabu vya watu tunaowaita Ahlullah...
Kama tuko sahihi
katika uchanganuzi huu; wale ambao anashindwa kuufanyia kazi mtazamo huu
wafikirie wenyewe ni mambo yapi zaidi wanayakosa!.
Kama tumepotoka;
basi tutaangamia vibaya sana katika mikono ya huyo Mungu aliyekaa pahali fulani
huko juu, ambaye mara moja kwa mwaka anawatuma malaika pamoja na roho duniani
katika kiza la usiku!..
AHMED HULUSI
2
September 2005
(Imetafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kituruki)
|