|
Siku
hizi kuna waliopewa ufahamu na wanaoonekana kana kwamba wamepewa ufahamu!.
Kunawasomi na wanaoonekana wasomi!.
Kunawashinikizaji na wanaotaka kushinikizwa!
Kuna
“ISLAM”; Kuna “Uislam”!.
Waliopewa ufahamu ni wale wenye kupata ukweli na kuuelewa baada ya kuchanganua
nyaraka kwa mtazamo ulio huru!. Wanaoonekana wamepewa ufahamu ni wale wenye
kujaribu kukusanya michango kwa kutumia yale waliyoyaelewa kutoka kwa wenye
ufahamu na kuuza kwa wale wanaowazunguka!.
Wapo
wasomi duniani... Wanaojitahidi kuchonga maisha yao kwa akili kwa kutumia fikira
za kisayansi! Wapo wanaoonekana wasomi; wanaoiga wasomi waliowavutia.
wanatamani kuvaa, kula, kunywa na kuzungumza kama wao!..
Ni
madini hewa yanayong’aa vichochoroni. Ung’avu wao unawasisimua hao
wavichochoroni!.. Lakini hawajapata kuona; hawajui tofauti kati ya kito cha
kweli na cha bandia. Kwa hiyo hawa ndio walengwa wa hayo madini bandia! Na wako
radhi kutoa vingi mno ili wafanane nayo, lakini hawatoweza hata kidogo!
Wapo
wanaopenda kushinikiza watu kwa sababu ya maumbile na uweza wao.. wanawaongoza
na kuwatawala watu; wanafanya hivi katika uelekeo wa kupata faida kimali au
kiroho!. Wanatengeneza vikundi kwa ajili ya kuvitawala, kuvipa amri na kukidhi
hamu yao ya ukamanda ambao wameshindwa kuufanikisha. Kwa upande mwingine wapo
wale wanaopenda kushinikizwa nakufanya utumishi ; wapo ambao kujiamini kwao
kunategemea hili; unyonge wao wameamua kuuonyesha katika namna hii!.
Hali ni
hii kila pahala duniani!
Ukweli
ni kwamba Allah amemuumba mtu kama kiumbe chenye hadhi ya juu kuliko vyote,
amejaalia awe Khalifa katika ardhi; Lakini nani anajali!.
Ndiyo!
hawa wanaoonekana wasomi wakishirikiana na wanaoonekana wamepewa ufahamu
wanaujadili uislam ambao hauna mantiki wala hauwiani na sayansi; Kwa kusisitiza
hali ya kubaki nyuma ya watu wanaoufuata “UISLAMU” wanadhani kwamba wanakosoa
“DINI YA ISLAM” !.
Watu
hawa kutokana na kutojua, hawafahamu tofauti kati ya “DINI YA ISLAM” na
“UISLAM”, na kwamba swala la dini haligusiki bila kufahamu tofauti hii!
Kwa
kuchukua mawazo yenye thamani ya madini bandia kana kwamba ndio wazo la msingi
wa dini ya ISLAM wanaacha madini yenyewe kutokana na kuta kujua.
Wanakosa
jinsi ya kufanya wenye kuhitaji kufunzwa; kwani vyanzo vya kujifunza
walivyonavyo ni uzushi wa wakandamizaji na maneno ya wapambe wao!...
Wanaiangalia Dini ya ISLAM kana kwamba ndiyo uislam wa wale watu wenye
kuchukulia MAULIDI kama ibada; wanaosherehekea Nyisiku zenye thamani; Wanaodhani
kwamba sharti la kwanza la kuwa muislam ni mwanamke kujifunika kichwa;
wanaodhani kwamba Swala na funga vimewekwa ili kumfurahisha mungu wa mawinguni
wa wapapatikiaji wa mungu wa mawinguni!.
Hawaelewi kwamba maulidi ni shairi liliandikwa na Suleyman Chelebi, na kwamba
haina uhusiano wowote na ibada zilizotajwa na Quran. Hawajabaini kwamba nyisiku
za Miraj, 15 Shabani, Qadir si kwa ajili ya kuwasha mishumaa kwa maiti wetu,
utaratibu ambao hauna uhusiano na Dini, bali ni nyisiku zenye masaa yenye
thamani... Hata hawajasikia ya kwamba hakuna sikukuu ya kuchinja na ya peremende
bali kuna ufanikishwaji wa sikukuu za FITR na HAJ. Hawajaelewa kwamba Swala,
Funga na Hija zinazoelezwa na Quran si kwa ajili ya kumfurahisha Mungu wa
Mawinguni bali ni kwa ajili ya kuokoa maisha yao ya baadae!
“DINI
YA ISLAM” ni mfumo na utaratiibu katika enzi ya Allah ulio juu ya wazo la muda!.
Ni chanzo, ni kiini, haibadiliki na wakati... Huu ndio ufafanuzi wa Quran!.
“UISLAM” ni
uchanganuzi wa watu wa dini ya ISLAM kutegemeana na uwezo wao, mashinikizo, mila
na desturi za mazingira yao ndani ya mipaka iliyowekwa na watawala wao.
Umefika
wakati wa kuelewa kwamba machanganuzi hayadhibiti Dini ya Islam!.. Jitahidini
kubaini kiini!.
Achaneni
na UISLAM na mtazame Dini ya Islam!
AHMED HULUSI
|