|
Lengo la uwepoji wa Mtu katika ardhi ni kuufanikisha kwa dhati
UKHALIFA...
Kuutumia ipasavyo UKHALIFA kunawezekana pale mtu atakapouelewa
undani wake yeye mwenyewe pamoja na asili yake; kisha akahisi na kufanikisha
yale yote yanayoambatana na UKHALIFA.
Njia ambayo mtu ataitumia kuufanikisha UKHALIFA ni kujikwamua
na kujitakasa kutokana na masharti ya mazingira ya alipozaliwa pamoja na kuacha
kutuhumu watu kwa mitazamo ya kidesturi, kisha kujitahidi kujipa MWENENDO WA
ALLAH.
Hautojulikana MWENENDO WA ALLAH bila kufahamu ipasavyo
LINALOKUSUDIWA NA JINA ALLAH!
Iwapo halitofahamika hili, basi mtu atatengeneza kichwani kwake
kiumbe CHA KUKIPAPATIKIA na kukipa jina la ALLAH; Kisha akakipa sifa na nyadhifa
mbalimbali kufuatana na shinikizo la mazingira yanayomzunguka, hisia zake
pamoja na desturi ya jamii yake. Mtu huyu ataondoka kutoka duniani akiwa mwenye
KUJILIWAZA kwa kujikagua na kujirekebisha kwa kadiri atakavyoweza kwa mujibu wa
huyo MUNGU aliyemtengeneza kichwani mwake.
Elimu ni CHOMBO cha kumuongoza mtu kufanya analopaswa
kulifanya!...
Kuufanikisha UKHALIFA ndiyo lengo la
uwepoji wa mtu!...
Yaani, lengo pekee la Mtu ambaye ameumbwa awe KHALIFA ni
kuvishinda vipangamizi vyote na hivyo kufanikisha UKHALIFA wake.
Kama mtu utashindwa kuondoa katika ufahamu wako, na kujikwamua
na yote ambayo kesho utalazimika kuyaacha, hutoweza kukipata kitambulisho chako
cha kweli.
Wakati huu tulionao MAMBO YA TARIQA hayapo tena. Yaani kwa maana
yake ya dhati, ule uhusiano kati ya SHEIKH na DARWESHI umefika mwisho; Ule
uhusiano wa MLEZI na MLELEWA umekwisha toweka!...
Mfano wa mahusiano haya ni kama ule wa YUNUS na TAPTUK!... YUNUS
Ndani la baraza la TAPTUK, aliloingia akiwa na miaka ishirini, anakandwa
ipaswavyo; anafunzwa namna ya kukaa mpaka kusimama; kula mpaka kunywa; maneno
anayotakiwa kuyasema mpaka namna ya kufikiria; kisha anaruhusiwa kurudi mtaani
kufanyia kazi aliyojifunza akiwa na miaka miaka sitini...
Jambo hili haliwezekani kwa wakati huu tulionao.
Hutoweza kumpata mtu wa kukusimamia kukurekebisha na kukuongoza
kila sekunde!...
Jitakaseni na kujikwamua kutokana na mambo ambayo asili yake ni
ndoto!..
Mtu hafunzwi tabia kwa kunyooshewa mkono kutoka mbali!..
Elimu inaweza kuruka kutoka mbali, China kwa mfano; Elimu hii
inanaswa na ubongo wowote wenye uwezo wa kupokea elimu hiyo, na kufanyiwa kazi.
Lakini mwenendo wako na mapungufu yote ya tabia hayarekebishiki kutoka mbali.
Hili ni jambo unaloweza kulifanikisha wewe mwenyewe kutegemeana na kiwango cha
elimu yako.
Uwezekano wa kurekebishika kwa hisia, tabia na mtazamo wako kwa
msukumo unaotoka mbali ni ndoto ya machana!
Mfumo huu ambao tupo ndani yake ni kazi ya sanaa ya MWENENDO WA
ALLAH!...
Quran ni kitabu tulichopewa ili tuweze kuutambua huu mfumo wa
ALLAH ambao tunaishi ndani yake...
Kama kwa namna yeyeto ile UELEWO wetu wa Quran hauwiani na
MTAZAMO wetu wa huu mfumo basi inamaanisha kwamba bado hatujai-SOMA Quran!
Quran inapoSOMEKA mfumo unabainika na hivyo kupelekea kubainika
kwa MWENENDO WA ALLAH...
Daraja la UKHALIFA WAKO linawiana na kiwango chako cha kuuvaa
MWENENDO WA ALLAH pamoja na uwezo wako wa kuchambua mambo kwa mujibu wa mtazamo
huo.
Hakuna fimbo itayotoka MAWINGUNI kuja kukufanya uwe KHALIFA au
WALII; kwani haya ni majina ya mwenendo na mtazamo katika maisha...
Kama wewe huna mwenendo au Mtazamo huu basi hautoweza kubadili
sifa uliyonayo hata kama ukijivisha kitambulisho chenye maandishi ya dhahabu cha
kukuonyesha wewe unasifa hizo.
Nawashauri “MSIZIDHULUMU NAFSI ZENU” kwa kujilaghai wenyewe na
matarajio ndoto!.
Kinachokufikiaeni ni elimu ambayo ndiyo Shifaa (Muombezi).
Kwa mujibu wa elimu hiyo mtachonga maisha na kujitahidi
kujikomaza...
Mtu mwenye Akili ni yule mwenye kufanya jitihada
kujikomaza(Kujiendeleza)... Hapotezi muda wake bure kwa kuhangaika na
wanaomzunguka katika mambo yasiyo muhimu!.. Kumbuka kwamba ni Faradhi kusambaza
unayoyajua!... Tabligh ni FARADHI... Hali kadhalika ni faradhi kutowalazimisha
watu katika jambo lolote lile baada ya kuwafahamisha.
Hivyo basi jukumu la kila mmoja wetu ni kunufaika na elimu kwa
moyo safi bila kufungwa na ndoto za mchana; Kuwakubali watu kama marafiki tuu na
kuzingatia ushauri wao bila kuwafanya masanamu ya kuyapapatikia; Kukubali ukweli
wa kwamba lolote litakalotusibu ni matokeo ya tuliyoyafanya, na hivyo basi
kujitahidi kuchonga njia zetu wenyewe bila kuwa na ndoto ya kuwatwika wengine
mizigo yetu...
ALLAH awe ameturahisishia kufanikisha yote kwa mujibu wa elimu!.
AHMED HULUSI
14.6.1998
New Jersey USA
Kutoka katika kitabu: WITO WA MFUMO
|