|
Tulipata kuandika kuhusu “Bismillah”
katika kitabu chetu cha MAMBO YA MSINGI YA UISLAM katika uchambuzi wa suratul
Fatiha; vile vile ndani ya makala yenye kichwa “RAHMAN - RAHIM”.
Hapa tutaangalia upande wake mwingine...
Inafahamika kwamba katika swala za jamaa pamoja na ukweli wa kwamba bismillah
ndiyo aya ya mwanzo ya suratul Fatiha, huwa haisomwi kwa sauti na imam!
Imam huwa anaanza kusoma kwa sauti moja kwa moja kuanzia na
“alhamdulillahirabbil’alamiyn”
Je ni kwa nini Imamu huwa hasomi bismillah kwa sauti pamoja na kuwa ndiyo aya ya
kwanza ya suratul fatiha na kusoma kwa sauti kuanzia aya ya pili? Na hapo
maamuma wanaisoma kimoyomoyo(!) eti kukamilisha mapungufu yake(!)
Kwanza ngoja tugusie kwa kifupi jambo ambalo lilijadiliwa zamani.
Wapo waliosema kwamba suratul fatiha ina aya 7; na wapo waliosema kwamba aya ya
kwanza ya suratul fatiha “alhamdulillahirabbil’alamiyn” na kwamba bismillah ya
mwanzo imewekwa kama kianzilishi tuu.
Wale waliozama katika jambo hili kwa undani wamefikia maoni ya kwamba bismillah
ndiyo aya ya kwanza ya suratul fatiha.
Na wengi wetuı hii leo tunamaoni kama hayo.
Hali ikiwa ni hiyo jambo linalotuvutia kwanza ni hili lifuatalo...
Kwa nini baada ya kusema “Rahmanirrahim” pamoja na Bismillah, ikarudiwa tena
baada ya “alhamdulillahirabbil’alamiyn”? Hatutoingia katika mjadala huu hapa.
Lakini kutokana na umihimu wa jambo hili tunataka kugusia kwa mara nyingine hizi
aya mbili kama ifuatavyo:
1. “Bismillahir Rahmanirrahim”
2. alhamdulillahirabbil’alamiyner Rahmanirrahim
Siri iliyopo hapa tumejaribu kuieleza katika makala yetu ya “RAHMAN - RAHIM” kwa
kadiri maneno yalivyo ruhusu.
Kwa mujibu wa ukweli huo, tunalotakiwa tulifahamu ni:
Ili swala igeuke kuwa Miraji ni lazima mtu, kwa kuielewe siri inayokusudiwa na
herufi “B”, aihisi KWA DHATI maana iliyokusudiwa na Bismillah!
Kwa hiyo, hata katika swala za jamaa, haitoshi imamu kusoma bismillah kwa niaba
ya maamuma! Inabidi mtu aanze swala kwa kuisoma mwenyewe bismillah kwa dhati na
hisia.
Yani, imamu hawezi kusema bismillah kwa niaba ya maamuma
Ili mtu aweze kuzama ndani ya sala inambidi achanganyike na ya Bismillah
Ni furaha iliyoje kwa mwenye kubahatika kuchanganyika na bismillah hata mara
moja kwa siku!
Wassalaam!.
AHMED HULUSI
10.3.2003
Raleigh - NC, USA
|